Star Tv

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya kasi i ya ujenzi wa barabara ya Bububu-Mahonda hadi Mkokotoni.

Dk. Shein aliyasema hayo huko katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini “A”, Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Wazee wa CCM wa Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja.

Katika maelezo yake Rais Dkt. Shein aliwaleza waliohudhuria katika mkutano huo kuwa kutokana na kasi hiyo kubwa ya ujenzi wa barabara hiyo yenye Kilomita za mraba 31 ana matarajio makubwa ya kuzinduliwa kwa barabara hiyo katika sherehe zijazo za Mapinduzi

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Abdalla Juma Mabodi alisisitiza kuwa CCM inathamini uwepo wa wazee na kueleza kuwa Serikali zote mbili zimeeleza jinsi zitakavyowajali wazee.

Kwa niaba ya wazee hao Naibu Mabodi alimpongeza Rais Dk. Shein kwa uamuzi wake wa kuwafuata wazee katika Wilaya zao Unguja na Pemba.

Dkt. Shein alieleza jinsi wananchi wa Wilaya ya Kaskazini A, walivyofarajika kwa ujenzi alioufanya wa Tawi lililoanza kujengwa na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume huko Mshezashauri pamoja na ujenzi wa Maskani mbali mbali za CCM katika Wilaya hiyo.z

Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo alitumia fursa hiyo kwa kumpongeza Rais Dk. Shein kwa kusimamia na kuuendeleza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sambamba na kuwepo kwa amani na utulivu mkubwa hapa nchini ambao umepelekea kuwepo kwa maendeleo endelevu.

Mwisho

Latest News

ZIMBABWE KUKABILIANA NA WANAOIPAKA TOPE NCHI YAO.
07 Aug 2020 16:05 - Grace Melleor

Taifa la Zimbabwe limesema lipo mbioni kupitisha sheria mpya ambayo itatoa adhabu kali kwa vyama vya kisiasa vinavyofany [ ... ]

MEMBE TAYARI AJIDHATITI KWA MAPAMBANO.
07 Aug 2020 15:35 - Grace Melleor

Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe tayari amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya M [ ... ]

MWANAMFALME WA SAUDI ASHUTUMIWA KWA KUTUMA MAMLUKI CANADA.
07 Aug 2020 15:21 - Grace Melleor

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameshutumiwa kwa kutuma mamluki nchini Canada ili kumuua aliyekuwa afisa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.