Serikali imesitisha kwa muda usiojulikana shughuli za uchimbaji wa Madini ya Dhahabu katika machimbo ya Shilalo wilayani Misungwi mkoani Mwanza ili kupisha uchunguzi wa mgogoro uliojitokeza baina ya kikundi cha Mlimani ambao ni waanzilishi wa uchimbaji, mmiliki wa shamba na mwekezaji mpya aliyejitokeza kuwekeza eneo hilo.
Ni baadhi ya wachimbaji wadogo katika Machimbo ya Shilalo yaligunduliwa na wachimbaji hao Mwaka 2017 yakiwa na yanajumla ya madura ya uchimbaji 57 ambapo 38 yamesitishwa na serikali kuendelea na uchimbaji huo.
Machimbo hayo yaliyositishwa tangu Oktoba Saba mwaka huu ,Chanzo cha mgogoro ni mmoja wa wamiliki wa shamba linalochimbwa kudaiwa kuweka mwekezaji mwingine huku wanakikundi cha Mlimani group wakiwa hawafahamu hatima yao.
Mmiliki wa Shamba hilo Wilbert Magwatamula amesema shamba hilo amelinunua tangu mwaka 1982 na anamtambua kikundi cha Mlimani kuwa ndio wawekezaji wa mwanzo.
SB: Wilbert Magwatamula Mmiliki wa Shamba
Meneja Msaidizi wa kikundi cha Mlimani Dastan Henry ambao ndiyo walioanza kuchimba machimbo hayo amebainisha chanzo cha Mgogoro huo na manufaa ambayo yanapatikana kutokana na machimbo hayo kwa wanakijiji.
SB: Dastan Henry - Meneja msaidizi wa kikundi cha Mlimani
Hata hivyo uongozi wa kijiji cha Shilalo bado unatia shaka na mwekezaji mpya anayedaiwa.
SB: Kang'wa Nzugamawe Sahani - M/Kiti wa Kijiji cha Shilalo
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ametoa kauli ya serikali wakati mgogo huo ukitafutiwa ufumbuzi .
SB: John Mongella - Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Machimbo ya Shilalo yanakadiriwa kuajiri wananchi elfu 6 wanaotegemea mgodi huo kuendesha maisha yao ya kila siku
Mwisho