Star Tv

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametoa muda wa siku 37 kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kuhakikisha ujenzi wa vituo vitatu vya afya vya Bereko, Thawi na Kalamba vinakamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Dkt. Kijaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini, ametoa maagizo hayo alipofanya ziara ya kutembelea mradi ya ujenzi wa vituo vya afya vinavyojengwa kwa fedha za Serikali katika vijiji mbalimbali Wilayani Kondoa, mkoani Dodoma, ambapo alibaini kuna uzembe katika umaliziaji wa ujenzi wa baadhi ya vituo hivyo kikiwemo Kituo cha Afya Kalamba. Ameelezea kutoridhika na utendajikazi wa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo katika usimamizi wa miradi hiyo muhimu kwa wananchi wakati Serikali ilikwishatoa fedha zote za kukamilisha miradi hiyo na kuagiza hadi Oktoba 30 mwaka huu miradi iwe imekamilika. “Dhamira njema ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli yakuleta milioni 400 kwenye kituo hichi cha Afya ni kupata huduma lakini hatujaanza kutoa huduma hiyo kwa zaidi ya mwaka sasa”, alisema Dkt. Kijaji. Ameagiza Ofisi ya Mkoa na Wilaya hukakikisha wanafuatilia vizuri utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi inayofadhiliwa na Serikali ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati kwa sababu Serikali haianzishi mradi mpya bila kutoa fedha zote za miradi husika. Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kondoa Bw. Mashauri Vicent alimuahidi Dkt. Kijaji kutekeleza magizo yote aliyoyatoa hasa ya kulipwa kwa watumishi waliofanya kazi mbalimbali kwenye vituo hivyo vya afya ndani ya siku 14. Dkt. Ashatu Kijaji alikuwa kwenye ziara ya siku mbili wilayani Kondoa, mkoani Dodoma ambapo ametembelea mradi wa Ujenzi wa vituo vitano vya afya wilayani huyo ambavyo vinajengwa kwa fedha za Serikali na kuahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wakazi wa Wilaya ya Kondoa.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.