Wakazi wa mji wa Maswa mkoani Simiyu wameilalamikia Mamlaka ya Maji na Usafi wa mazingira, (MAUWASA), kwa kitendo cha kupiga marufuku wamiliki wa mabomba ya maji kutoa huduma ya maji kwa watu wasiokuwa na huduma hiyo.
Baadhi ya waananchi wasiokuwa na mabomba ya maji wameilalamikia maamlaka ya maji kuweka zuio la kupata huduma ya maji kwa ndugu na jamaa zao. Hali ambayo wamesema inawaweka katika wakati mgumu kupata huduma ya maji safi na salama kutokana na wao kutokuwa na uwezo wa kumiliki mabomba ya maji katika makazi yao. Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira mjini Maswa (MAUWASA), Anacleth Tibita amewataka watu wasiokuwa na uwezo wa kumiliki mabomba ya maji kupata huduma hiyo katika vituo vilivyopangwa. Kwa siku za hivi karibuni mamlaka ya maji mjini maswa imekuwa ikifanya msako wa kusitisha huduma ya maji kwa wateja wake wanaotoa maji kwa watu wasiokuwa na huduma hiyo.