Star Tv

Upelelezi wa kesi ya utakatishaji fedha wa Dola za Kimarekani Milioni 6 inayomkabili aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Harry Kitilya na wenzake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bado haujakamilika ikiwa ni mwaka mmoja na nusu sasa.

Mbali ya Kitilya, Washtakiwa wengine ni aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1996 ambae pia ni Ofisa wa Stanbic Bank, Shose Sinare na Sioi Graham Solomon ambao walifikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza April 1,2016 kwa kukabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha.

Wakili Mwandamizi wa Serikali Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba wanasubiri awamu ya pili ya upelelezi kutoka Uingereza hivyo akaomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine.

Baada ya kuelezwa hayo, Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi November 10,2017 ambapo kwenye kesi hii, Washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya March 2013 na September 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani 550 milioni kwa serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Uingereza.

Pia wanadaiwa kuwa March 2013 Dar es Salaam walijipatia Dola za Marekani Milioni 6 wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia Kampuni ya Egma T Ltd.

Latest News

Rais John Magufuli atembelea majeruhi wa ajali ya moto Muhimbili.
11 Aug 2019 16:07 - Kisali Shombe

Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewatembelea majeruhi 43 wa ajali ya moto iliyotokea Agost [ ... ]

Waziri Mkuu akerwa na upandishwaji wa bili ya maji, Maswa.
09 Aug 2019 11:44 - Kisali Shombe

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekerwa na kitendo cha Mamlaka ya Maji wilayani Maswa kupandisha bili ya maji kutoka sh 5, [ ... ]

Raia kutoka nchini China watumikia kifungo cha miaka 18 au faini milioni 315
09 Aug 2019 11:29 - Kisali Shombe

Mahakama ya hakimu mkazi Tarime mkoani Mara imewahukumu kifungo cha miaka 18 jela ama kulipa faini ya shilling million 3 [ ... ]

Other Articles

Social Media

Star Tv - Advertisement
Star Tv - Advertisement
Star Tv - Advertisement

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.