Star Tv

Asasi Isiyo ya kiserikali inayojihusisha na kupinga Ukatili kwa wanawake na watoto mkoani Kigoma KIWODE ikishirikina na Vyombo vya Dola na wadau wengine imezindua na kuanza kutekeleza mpango wa kupinga na kukabIlina na vitendo vya ukatili na ubakaji vinavyotajwa kuanza kuota mizizi ndani ya manispaa ya Kigoma Ujiji.

Vitendo hivyo vimekuwa vikihusishwa na imani za kishirikina. Mkakati huu unahusisha ,jeshi la polisi ,Viongozi wa Serikali za mitaa viongozi wa Dini na wananchi wa kawaida unatarajiwa kuwa chachu ya kuyabaini maeneo
na watu wanaoendesha vitendo hivyo na kufikishwa katika mamlaka za kisheria.Jeshi la Polisi limeahidi kutoa ushirikiano mkubwa katika suala hilo, huku idara ya maendeleo ya jamii manispaa ya kigoma katika mpango huo ikijikita katika suala la uelimishaji umma. Kata zinazotajwa kukithiri kwa vitendo vya aina hiyo ya ubakaji ambako mpango huo utaanza kutekelezwa ni, Bangwe, Mwanga kaskazini, Kibirizi, Matubukana na Mwanga kusini.

Latest News

WATU WATANO WAFARIKI BAADA 'KUSHIKWA MATEKA' KANISANI.
11 Jul 2020 16:57 - Grace Melleor

Watu watano wameuawa baada ya washambuliaji kuvamia kanisa moja Afrika Kusini wakati malumbano yanaendelea juu ya uongoz [ ... ]

RAIS MAGUFULI AMTEUA MAMA SAMIA KUWA MGOMBEA MWENZA.
11 Jul 2020 16:21 - Grace Melleor

Rais Magufuli amemchagua Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea mweza katika Uchaguzi wa Urais wa Tanzania, Oktoba 2020.

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.