Star Tv

Wajumbe kutoka baraza tawala la kijeshi la Sudan na muungano mkuu wa upinzani wamepiga hatua kuhusu masuala tata katika mazungumzo ya kuyahamisha madaraka kutoka utawala wa kijeshi.

Mazungumzo ya namna ya kuiongoza nchi hiyo baada ya kuangushwa kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir yalisitishwa Jumanne baada ya kuuawa watu saba katika maandamano siku ya Jumatatu, wanne kati yao wakiwa watoto. Lakini jana, Khalid Omar, kutoka muungano wa Forces for Freedom and Change - FFC, alisema kamati zao za kiufundi za ngazi ya chini zimeyaorodhesha masuala muhimu yanayozusha utata, katika tamko la kikatiba ambalo litaweka njia kutoka utawala wa kijeshi hadi kwa baraza kuu jipya. Omar ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa makundi ya ngazi ya juu yatakutana kwa mazungumzo zaidi katika kipndi cha saa 48. Hata hivyo hakutoa maelezo kuhusu masuala yaliyokubaliwa.

CHANZO: Idhaa ya Kiswahili DW

Latest News

WATU WATANO WAFARIKI BAADA 'KUSHIKWA MATEKA' KANISANI.
11 Jul 2020 16:57 - Grace Melleor

Watu watano wameuawa baada ya washambuliaji kuvamia kanisa moja Afrika Kusini wakati malumbano yanaendelea juu ya uongoz [ ... ]

RAIS MAGUFULI AMTEUA MAMA SAMIA KUWA MGOMBEA MWENZA.
11 Jul 2020 16:21 - Grace Melleor

Rais Magufuli amemchagua Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea mweza katika Uchaguzi wa Urais wa Tanzania, Oktoba 2020.

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.