Star Tv

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga  ametembelea na kujionea maandalizi ya Maadhimisho ya 27 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane) yenye lengo la kuwatambua na kuwaenzi Wadau Wakuu wa Sekta ya Kilimo ambao ni Wakulima, Wafugaji, Wavuvi, Wanaushirika, Wasindikaji wa mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na maliasili kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa katika kuendeleza uchumi wa nchi yetu. 

Mhe Hasunga pamoja na mambo mengine akiwa katika Banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ameutaka uongozi wa taasisi  huyo kuongeza juhudi za utoaji elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa matumizi ya mifuko maalumu ya kuhifadhia nafaka ya PIC'S.

Mhe Hasunga amesema kuwa NFRA inapaswa kutoa elimu hiyo ili iwafikie wakulima wengi kwani kufanya hivyo itarahisisha huduma za uhifadhi wa mahindi ya wakulima ambao kwa muda mrefu wamekumbwa na kadhia ya kushindwa kuhifadhi mahindi kwa ufasaha.

Pamoja na NFRA kutoa elimu kwa wakulima kupitia vipindi mbalimbali vinavyorushwa na Televisheni lakini pia amesisitiza kuwa NFRA inapaswa kuongeza uwezekano wa kuwafikia wakulima wengi zaidi.

Mwaka huu wa 2019, sherehe za Nanenane zinafanyika Kitaifa mjini Bariadi katika Viwanja vya maonesho ya kilimo Nyakabindi katika Mkoa wa Simiyu hivyo Mhe Hasunga amepongeza Uongozi wa mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara kwa juhudi zao za kufanikisha kuingiza uwanjani huduma za msingi ambazo ni maji na umeme.

Alisema kuwa jukumu hilo kwa Serikali na Wadau wa Sekta Binafsi ni kuendeleza viwanja hivyo vya Nyakabindi kwa kujenga mabanda ya maonesho ya kudumu na kuboresha huduma muhimu za kijamii ili kuwe na maonesho endelevu yenye sura ya Kitaifa na Kimataifa.

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA pamoja na Taasisi zingine za wizara ya Kilimo zimetuama Mkoani Simiyu kwa ajili ya kutoa elimu kwa wakulima kuhusu majukumu wayafanyayo kadhalika namna bora ya kuwa na Kilimo bora na chenye tija.

Latest News

Kumbukumbu ya miaka 20 ya Hayati Mwalimu Nyerere
14 Oct 2019 12:52 - Kisali Shombe

Kila tarehe 14/10 Tanzania inaazimisha kumbukumbu ya kifo cha hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwa [ ... ]

Mgogoro machimbo ya Shilalo Mwanza: Serikali yasitisha uchimbaji wa Dhahabu
11 Oct 2019 10:14 - Grace Melleor

Serikali imesitisha kwa muda usiojulikana shughuli za uchimbaji wa Madini ya Dhahabu katika machimbo ya Shilalo wilayani [ ... ]

Kesi Ya Uhujumu Uchumi: Sethi Na Rugemalira Waandika Kuomba Msamaha
11 Oct 2019 09:46 - Grace Melleor

Hayo yamebainika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imeeelezwa, Seth aliandika barua yake iliyopitia kwa Mkuu [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.