Star Tv

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka, ameitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA,  kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya kutumia vyakula, vipodozi  na dawa zilizokwisha muda wake wa matumizi. Ilikuwa ni kikwazo kwa wajasiriamali wadogo mkoani Simiyu kufuata huduma za Mamlaka ya Chakula  Dawa TFDA jijini Mwanza, lakini kwa sasa wamesogezewa huduma karibu mjini Bariadi, pamoja na kupongeza hatua hii, changamoto hazikosekani.

TFDA imezindua ofisi mjini Bariadi kwa ajili kusogeza huduma kwa wananchi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa Mashariki ambayo ni Simiyu, Mara na Shinyanga, ambapo Kaimu Meneja wa Kanda hiyo Nuru Mwasuluma anaelezea namna walivyojipanga kutoa huduma, kubwa kudhibiti ubora na usalama wa vyakula, vipodozi na dawa.

Aidha Mtaka amesisitiza mamlaka hiyo kuangazia zaidi maeneo ya vijijini ambayo kwa muda mrefu yamesahaulika, huku wananchi wakiwa kwenye hatari ya kuuziwa na kutumia bidhaa zilizomaliza muda wake wa matumizi.

Latest News

ZANZIBAR YAFUNGUA MILANGO KWENYE UTALII.
06 Jun 2020 10:30 - Grace Melleor

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeruhusu kuanzia leo safari za ndege za kitalii kuwasili nchini baada ya mambukizi ya [ ... ]

UFARANSA YATANGAZA KIFO CHA KIONGOZI WA AL-QAEDA.
06 Jun 2020 08:27 - Grace Melleor

Waziri wa Jeshi wa Ufaransa Florence Parly ametangaza kifo cha kiongozi wa al-Qaeda katika ukanda wa Maghreb (Aqmi) Abde [ ... ]

MZOZO WA SERIKALI YA LIBYA NA HAFTARI WAENDELEA KUSHIKA KASI.
06 Jun 2020 07:20 - Grace Melleor

Serikali ya Libya yadai kuuteka mji muhimu kutoka kwa hasimu wake Khalifa Haftar.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.