Madiwani halmashauri ya wilaya ya bariadi mkoani Simiyu wameilalamikia serikali kuhusu zao la pamba kukosa soko la uhakika na hivyo kumdidimiza mkulima.

malalamiko hayo wameyatoa katika mkutano wa baraza la madiwani wa kujadili na kupitisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo ngazi za kata.

Wanaona kukosekana kwa soko la uhakika la zao la pamba kunamsababishia hasara mkulima aliyotumia wakati wa kilimo jambo ambalo linakuwa kinyume na kauli mbiu ya ‘Pamba ni Dhahabu Nyeupe.

Huku bi Penina mponeja diwani viti maalumu kutoka kata ya Dutwa ameitaka serikali kuchukua hatua kwa wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la machinga kulangua pamba ya wakulima kwa bei tofauti na ile elekezi.

Latest News

Kiwanda cha Alizeti chakosa malighafi, Mara
17 Jul 2019 13:12 - Kisali Shombe

Halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara imetenga zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano ili kuwapa wakulima  [ ... ]

Mtendaji awekwa ndani kwa kula fedha za vitambulisho.
16 Jul 2019 14:01 - Kisali Shombe

Mkuu  wa  wilaya  ya  Kalambo Julieth Binyura  amemweka ndani  kwa muda  wa  saa 24 mtendaji  wa  kijiji cha  [ ... ]

Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na M...
16 Jul 2019 12:49 - Kisali Shombe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2019 k [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.