Wananchi  katika   kjiji cha  Kisungamile  kata  ya  matai   wilayani  Kalambo  mkoani  Rukwa  wameiomba  serikali  kufanya   marekebisho  ya   miundombinu  ya  maji  ambayo  imeharibiwa  na mifugo  na  hivyo  kupelekea  kukosekana kwa  huduma hiyo muhimu    kwa zaidi  ya mwezi  mmoja  na  hivyo  kulazimika  kutumia  maji  ya  visima  ambayo ni  hatari  kwa  afya  zao.

Kijiji  cha  kisungamile  kina  zaidi   ya  wananchi  elfumoja  (1000)  na  kina patikana   katika  kata  ya  Matai , kijiji  hiki  kimekuwa  kikikabiliwa  na  changamoto   kubwa  ya  ukosefu  wa  huduma  ya  maji na  huku  wananchi wake  wakilazimika  kutumia  maji  ya  mto Chimilango  pamoja  na  maji  ya visima  ambayo  si salama  kwa  afya  zao na  hivyo  kulazimika  kuitisha  mkutano  wa hadhara  ili  kujua  hatima  ya  swala  hilo.

Diwani  wa  kata   hiyo  Vitus  Tenganamba  amesema  serikali  inampango  wa   kuanzisha  mradi  mpya  wa  maji   kwenye  maeneo   hayo   na  kuwataka  wananchi  kuendelea  kuwa  na subira  wakati  swala  lao  likiendelea  kufanyiwa  kazi. Mkuu wa  wilaya  hiyo Julieth  Binyura  amewataka  wananchi  kuacha  kulima  kwenye  vyanzo  vya  maji kwa  lengo  la  kuondokana na adha   kuziba  kwa  mabomba  hususani  wakati  wa  masika. Inaelezwa  kuwa   chanzo  cha  kukatika  kwa  maji  kila  wakati  kwenye  maeneo  hayo  ni  kutokana na  wananchi  kulima  kwenye vyanzo  vyamaji na   huku  maji  yanayotoka   yakiwa  ni  machafu  muda  wote.

 

Latest News

Kiwanda cha Alizeti chakosa malighafi, Mara
17 Jul 2019 13:12 - Kisali Shombe

Halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara imetenga zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano ili kuwapa wakulima  [ ... ]

Mtendaji awekwa ndani kwa kula fedha za vitambulisho.
16 Jul 2019 14:01 - Kisali Shombe

Mkuu  wa  wilaya  ya  Kalambo Julieth Binyura  amemweka ndani  kwa muda  wa  saa 24 mtendaji  wa  kijiji cha  [ ... ]

Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na M...
16 Jul 2019 12:49 - Kisali Shombe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2019 k [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.