Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Uvinza imetoa onyo kwa wajumbe wa kamati ya usimamizi wa mpango wa TASAF Ngazi ya vijiji CMC kuchukua pesa zinazotolewa za kuwalenga
wanufaika wa TASAF na kuzitumia kinyemela na kuahidi kuchuku hatua kali za kinidhamu na Kisheria kwa mtu yeyote atakaye bainika kufanya hivyo.

Kamati hiyo ya ulinzi na usalama wilaya ya Uvinza imetoa Onyo hilo huku kukiwa na kumbukumbu ya hapo mwaka jana kukamatwa na  kutiwa hatiani kwa Wajumbe wa kamati ya usimamaizi ya TASAF ngazi ya kijijji katika kata za Ilagala na Muleala wilayani humo baada ya kubainika kutumia nafasi zao kusainia na kuchukulia pesa za Wanufika. Onyo hilo limetolewa kupitia mikutano ya hadhara Kwa wanufakia wa TASAF katika vijiji vya Nguruka Bweru na Nyagambo wilayani Uvinza wakati ziara ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Ilipopita kukagua utekelezaji wa TASAF. Huku mratibu wa TASAF halmashauri ya wilaya ya Uvinza Dismas Clement amelazimika kutoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya baadhi ya wanufaikia kuwepo Upendeleo katika utoaji wa Ruzuku.

Latest News

Kiwanda cha Alizeti chakosa malighafi, Mara
17 Jul 2019 13:12 - Kisali Shombe

Halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara imetenga zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano ili kuwapa wakulima  [ ... ]

Mtendaji awekwa ndani kwa kula fedha za vitambulisho.
16 Jul 2019 14:01 - Kisali Shombe

Mkuu  wa  wilaya  ya  Kalambo Julieth Binyura  amemweka ndani  kwa muda  wa  saa 24 mtendaji  wa  kijiji cha  [ ... ]

Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na M...
16 Jul 2019 12:49 - Kisali Shombe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2019 k [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.