Zaidi ya asilimia 80 ya  watoto  wenye umri wa chini ya miaka mitano, wamepatiwa chanjo ya  Surua Rubella  katika halmashauri ya Wilaya ya Singida kwa kipindi cha kuanzia Januari  hadi  machi mwaka huu.

Mratibu wa Chanjo katika halmashauri hiyo Emmanuel Mawa anasema kuwa kwa kipindi hicho walilenga kuchanja watoto 2,648 lakini wakafanikiwa kuwapatia huduma hiyo watoto 2,345 sawa na asilimia 89, mbali na surua rubella, pia penta wametoa chanjo ya  penta kwa  watoto 2,571 sawa na asilimia  97 kwa lengo la kuwafikia watoto 2,648 na kuwapatia huduma hiyo ya chanjo bure. Hata  hivyo amesema kuwa licha ya mafanikio hayo,  lakini  bado kuna changamoto ya  baadhi ya wazazi na walezi  kutojitokeza kuwapeleka watoto wao kwenye chanjo za aina mbalimbali, hali inayosababisha malengo yanayowekwa na halmashauri katika utoaji wa huduma hiyo kutofikiwa kwa asilimia 100.Wawa ametoa mwito  kwa wazazi na walezi kuachana na  imani  potofu na  kujenga utamaduni wa kuwapeleka watoto wao kwenye chanjo ili waweze kupata huduma hiyo kwani inatolewa bila malipo  na ni salama na muhimu kwa ajili ya kuwakinga watoto dhidi ya  magonjwa mbalimbali hatari.

Latest News

Kiwanda cha Alizeti chakosa malighafi, Mara
17 Jul 2019 13:12 - Kisali Shombe

Halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara imetenga zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano ili kuwapa wakulima  [ ... ]

Mtendaji awekwa ndani kwa kula fedha za vitambulisho.
16 Jul 2019 14:01 - Kisali Shombe

Mkuu  wa  wilaya  ya  Kalambo Julieth Binyura  amemweka ndani  kwa muda  wa  saa 24 mtendaji  wa  kijiji cha  [ ... ]

Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na M...
16 Jul 2019 12:49 - Kisali Shombe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2019 k [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.