Mahakama kuu kanda ya Musoma mkoani Mara imeanza kusikiliza kesi 15 za mauaji ya kukusudia na yasiyo ya kukusudia toka kwa watuhumiwa mbali mbali waliopo ndani ya magereza kwa muda wa wiki moja zikiwemo kesi nane toka mahakama kuu kanda ya Mwanza zilizokuwa zimeelekezwa huko ili ziweze kusikilizwa na kutolewa maamuzi.

Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Musoma mkoani Mara,mheshimiwa John Kayoza amesema kuwa wanataraji kusikiliza kesi 15 za mauaji ambazo zilifunguliwa awali lakini na mpya ambazo zimefunguliwa tokea mwezi wa pili mwaka huu. 'Ujio wa mahakama kuu kanda ya Musoma mkoani Mara unataraji kuwasaidia wananchi waliokuwa wakishindwa kwenda jijini Mwanza kuudhulia vikao vya kesi kutokana na kutokuwa na fedha za kuwawesha kufanya hivyo na sasa serikali imewasogezea huduma hiyo muhimu jirani yao, amesema Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dk, Vicenty Aney. Mahakama kuu kanda ya Musoma Mara imeanza kikao chake cha kwanza cha kusikilizxa kesi kumi na tano za mauaji huku ikitaraji baada ya wiki mbili kuketi na majaji watatu kusikiliza kesi mbali mbali zilizotoka kanda ya mwanza na kuzitolea maamuzi.

  

Latest News

Kiwanda cha Alizeti chakosa malighafi, Mara
17 Jul 2019 13:12 - Kisali Shombe

Halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara imetenga zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano ili kuwapa wakulima  [ ... ]

Mtendaji awekwa ndani kwa kula fedha za vitambulisho.
16 Jul 2019 14:01 - Kisali Shombe

Mkuu  wa  wilaya  ya  Kalambo Julieth Binyura  amemweka ndani  kwa muda  wa  saa 24 mtendaji  wa  kijiji cha  [ ... ]

Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na M...
16 Jul 2019 12:49 - Kisali Shombe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2019 k [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.