Star Tv

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemkuta na kesi ya kujibu mshtakiwa Salum Njwete maarufu kama Scorpion anaekabiliwa na kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi ambae aliingia kwenye vichwa vya habari baada ya kumtoboa mtu macho.

Hatua hiyo inatokana na Hakimu Mkazi Flora Haule kusema kuwa amepitia ushahidi wa upande wa mashtaka na kujiridhisha na kuona mshtakiwa Njwete ana kesi ya kujibu.

Hakimu Haule amesema kwa sababu hizo, Mshtakiwa anapaswa kutoa utetezi kwa njia atakazopenda kama kwa kiapo ama bila kiapo ambapo baada ya kueleza hayo, Mshtakiwa Njwete alisema kuwa atajitetea mwenyewe kwa njia ya kiapo lakini pia atakuwa na mashahidi wawili ambao walitumiwa kama Mashahidi wa upande wa mashtaka jambo ambalo Hakimu Haule amelikataa na kusema atafute mashahidi wengine au ajitetee mwenyewe.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Njwete anaetetewa na wakili Juma Nassoro anaidaiwa Septemba 6, 2016 saa 4 usiku maeneo ya Buguruni Ilala Dar es Salaam, aliiba cheni ya Silva yenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh 60,000 na simu ya mkononi pamoja na fedha taslimu Sh 330,000 vyote vikiwa na thamani ya Sh 474,000 mali ya Said Mrisho Said.

Pia anadaiwa kabla na baada ya kutekeleza tukio hilo, Mtuhumiwa huyo alimchoma Mrisho sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo machoni, tumboni na mabegani ili kurahisisha kupata mali hizo.

Hakimu Haule ameahirisha kesi hiyo hadi November 14, 2017 kwa ajili ya Njwete kuanza kujitetea.

Latest News

Rais John Magufuli atembelea majeruhi wa ajali ya moto Muhimbili.
11 Aug 2019 16:07 - Kisali Shombe

Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewatembelea majeruhi 43 wa ajali ya moto iliyotokea Agost [ ... ]

Waziri Mkuu akerwa na upandishwaji wa bili ya maji, Maswa.
09 Aug 2019 11:44 - Kisali Shombe

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekerwa na kitendo cha Mamlaka ya Maji wilayani Maswa kupandisha bili ya maji kutoka sh 5, [ ... ]

Raia kutoka nchini China watumikia kifungo cha miaka 18 au faini milioni 315
09 Aug 2019 11:29 - Kisali Shombe

Mahakama ya hakimu mkazi Tarime mkoani Mara imewahukumu kifungo cha miaka 18 jela ama kulipa faini ya shilling million 3 [ ... ]

Other Articles

Social Media

Star Tv - Advertisement
Star Tv - Advertisement
Star Tv - Advertisement

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.