Star Tv

Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza imeanzisha mchakato wa kuwakamata vijana wanaoonekana na wanafunzi wa kike katika vichochoro ama maeneo mengine yanayotia mashaka ya mahusiano ili kunusuru vijana na kadhia ya kupata ujauzito.

Akizungumza na wazazi pamoja na walezi wa watoto waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule ya sekondari ya Nyehunge, Mkuu wa wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole ameahidi kulisimamia suala la watoto wa kike kupata ujauzito katika umri mdogo, jambo ambalo linawanyima nafasi ya kupata masomo.

Amewataka wazazi na walezi kushiriki moja kwa moja katika malezi ya vijana wao wa jinsi zote Ili kutoa fursa ya wanawake kushika madaraka, baada ya kupata elimu. Shule ya sekondari Nyehunge iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa inaanzisha masomo ya kidato cha tano na sita ili kutoa nafasi pana kwa vijana kuifikia elimu ya juu, ingawa bado inakabiliwa na changamoto kadhaa.

Shule ya Sekondari Nyehunge imepokea wanafunzi wa chaguo la pili katika Tahasusi za CBG na HGL wakiwa wavulana 42 na wasichana 39, wanafunzi walioripoti hadi sasa ni 65 sawa na asilimia 80.

Picha na mtandao

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.