Star Tv

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afungua mashindano ya AFCON U17 na kutangaza kuwa kuanzia leo Watanzania wataingia bila kulipia.

 Alitoa kauli  hiyo kwenye ufunguzi wa michuano hiyo iliyoanza jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa michuano hiyo, aliambatana na Rais wa Shirikisho la Soka na barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad kukagua timu zilizofungua dimba na kisha kutangaza uamuzi huo wa Serikali. 

 Timu zilizofungua dimba ni Serengeti Boys ya Tanzania na Nigeria. Katika mchezo wa huo Nigeria ilibuka kidedea baada ya kuifunga Tanzania mabao 5-4. Hadi mapumziko timu ya Nigeria ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-1.

 

Mabao ya Nigeria yalipatikana dakika ya 20, 29, 36, 71 na 78 wakati mabao ya Tanzania yalipatikana dakika ya 21, 51, 56 na 60 ambapo magoli mawili kati ya hayo, yalipatikana kwa njia ya penati. Bao la kwanza la Tanzania lilifungwa na Alphonce Mabula Msanga  dakika ya 21. Bao la pili, lilipatikana dakika ya sita ya kipindi cha pili na lilifungwa na Kelvin Pius John.

 Dakika tano baadaye, Morice Michael Abraham aliipatia Tanzania bao la tatu lililofungwa kwa njia ya penati. Kabla vijana wa Nigeria hawajakaa sawa, dakika nne nyingine, Edmund Godfrey John alitinga kimiani bao la nne, ambalo pia lililifungwa kwa penati.

Timu ya Tanzania iko kundi A na imepangwa na timu za Nigeria, Uganda na Angola. Michuano hii inatarajiwa kumalizika Aprili 28. Endapo timu hiyo ya Taifa ya vijana ya Serengeti Boys itaibuka na ushindi katika michezo yake miwili, itakuwa imekata tiketi ya kushiriki mashindano ya dunia kwa vijana wa umri wa miaka 17 yatakayofanyika mwakani huko Brazil.

 

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.