Star Tv

Gari Moshi ya   mizigo  iliyobeba shehena  ya ngano iliyokuwa inatokea  Dar es Salaam kuelekea mikoa ya kanda ya ziwa mpaka Kampala nchini Uganda  imepata ajali  usiku wa kuamkia Aprili  kumi na tatu  katika eneo  la  Kola Manispaa ya Morogoro na kusababisha adha  kubwa kwa  wasafiri wanaotumia  njia hiyo kutokana na reli ya njia hiyo  kung’oka kabisa.

Ajali  hiyo inatajwa kutokea  Majira ya saa mbili  na robo Usiku na kusababisha njia hiyo ya reli kungoka na kusababisha treni nyingine kushindwa kupita katika eneo hilo. 

Akizungumza na waandishi wa habari  mkuu wa kituo cha reli mkoa wa Morogoro Bwana Salvatory kimaro  amesema  gari moshi hiyo ilikuwa na  injini namba  C261  ilikuwa na behewa ishirini  ambapo kati ya hazo mabehewa matano  yaliancha njia na kuanguka  ambapo   amesema chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika  hata hivyo hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa binadamu amebainisha mkuu wa kituo.

Baadhi ya wakazi wa morogoro ambapo wameiomba serikali  kuangalia kwa makini eneo kabla  hayajatokea madhara kwa binadamu  kwani  limekuwa likisababisha ajali mara kwa mara jitihida za mafundi  kurudisha tena njia hiyo ya treni ilikuwa ikiendelea .

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.