Star Tv

WANAWAKE nchini wametajwa kuwa ni nguzo imara katika ukuaji wa uchumi, kwa madai kuwa harakati zao ni chachu ya maendeleo, na hivyo kutakiwa kujikita katika shughuli zenye faida kubwa, ili gurudumu hilo la maendeleo kuuelekea uchumi wa viwanda lisukumwe kwa nguvu ya pamoja na watanzania wote.

Ni wanawake wajasiriamali wadogo wa mjini Iringa, wanaojishughulisha na biashara mbalimbali za kiuchumi, huku wengi wao wakielekeza nguvu zao katika biashara ndogondogo, na sababu kuu inayotajwa na wajasiriamali kubaki katika biashara hizi duni ni uhaba wa mitaji, unaowasababishia wao kukopa katika taasisi za kifedha zenye riba kubwa ambazo zinatajwa kudumaza mitaji ya wafanyabiashara wadogo Wajasiriamali wengine matamanio yao ni makubwa lakini kikwazo hapa ni namna ya upatikanaji wa mitaji.

Zainab Nuhu Mwamwindi ni mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWT Mkoa wa Iringa, yeye anawahimiza wajasiriamali wanawake kamwe kutobweteka kwa kufanya shughuli hizi zenye faida kiduchu na badala yake wajitoe kimasomaso kufanya biashara kubwa.

Zainab Mwamwindi ameyasema haya wakati umoja wa wanawake UWT mkoa wa Iringa ikitoa pongezi kwa rais John Magufuli, ambapo UWT amesema inaziona jitihada mbalimbali za rais ambazo zote zimekuwa na lengo la kupigania ukuaji wa uchumi wa Taifa la Tanzania.

Picha na mtandao

Latest News

KARATE: Rutashobya aomba serikali iruhusu Karate kufundishwa mashuleni
10 Dec 2019 12:32 - Grace Melleor

Bingwa wa Dunia wa Mchezo wa Karate Rutashobya Rwezahula¬† amesema Tanzania inaweza kutoa Mabingwa wengi katika Mchezo h [ ... ]

WANANCHI WANAOTOA NUSU YA FEDHA: Meneja TANESCO Pwani aagizwa kuwaunganishia ume...
10 Dec 2019 11:46 - Grace Melleor

Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu amemuagiza Meneja wa Shirika la Umeme nchini TANESCO mkoa wa Pwani¬†Martin Maduu ku [ ... ]

UKOSEFU WA MAFUTA MAALUM: Walemavu wa ngozi hatarini kupata Saratani
10 Dec 2019 11:38 - Grace Melleor

Walemavu wa Ngozi wanaoishi wilayani Monduli mkoani Arusha wapo hatarini kupata saratani ya Ngozi kutokana na kukosa maf [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.