Katika  jitihada  za kukabiliana  na  uvamizi  wa  tembo  kwenye  mashamba  ya   wananchi    mkoani  Rukwa, wakala  wa    hidfadhi za mistu  wilayani  kalambo  wameanzisha  mradi  wa  ufugaji  nyuki  ambao  utasaidia   wananchi  kujikwamua  na  hali  ya  kiuchumi  sambamba  na kufukuza  tembo kwenye mashamba   yao.

Kumekwepo  na malalamiko   ya  muda  mrefu  kutoka  kwa   wananchi  wa   kata  za Kisumba  na  Pombwe   wilayani  Kalambo   juu  ya  tembo  kuvamia  mashamba  yao  kisha   kuharibu  mazao na  kupelekea   serikali  wilayani  humo  kupitia  wakala   wa  hifadhi  za misitu  kubuni  njia   mpya   ya  kupambana  na  tembo hao kwa  kuanzisha  mradi  wa  ufugaji  nyuki.

Hayo yameelezwa wakati akisoma  akisoma  risala  fupi  mbele   ya  kiongozi   wa   mbio  za Mwenge Venansi  Sinkala  wakati  wa  uzinduzi  wa  mradi  huyo unayo shirikisha  vikundi vitano , amesema mizinga 100 yenye thamani  ya  shilingi  million  nane  imekwisha  kutundikwa   tayari.

kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru, haji abdulla hamad amewashauri wananchi kuendelea kutumia mbinu mbadala za kutumia misitu kwa faida kama kufuga nyuki ili kutunza vyanzo vya maji ili kufikia malengo ya serikali ifikapo mwaka 2025.Awali  akiupokea  mwenge  huo . mkuu  wa  wilaya  ya  Kalamnbo  Julieth  Binyura , amesema   mwenge  wa  uhuru  utazindua   miradi  9 yenye thamani  yua  shilingi  billion  1.2.

Latest News

Rais wa zamani wa argentina, afunguliwa mashitaka ya rushwa.
22 May 2019 09:10 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Argentina Cristina Fernandez de Kirchner amefunguliwa mashitaka ya rushwa, siku tatu baada ya kutangaz [ ... ]

Waziri wa mambbo ya nje akutana na Jumuia ya Mabohora
18 May 2019 14:03 - Kisali Shombe

Jumuia ya Mabohora Nchini imesema imeanza jitihada za kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania D [ ... ]

Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara kufungiwa kamera.
18 May 2019 13:48 - Kisali Shombe

Uongozi wa Hospital ya rufaa ya mkoa wa Mara umelazimika kufunga kamera maalumu katika maeneo yote ya hospitali hiyo ili [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.