Star Tv

Kikosi cha usalama barabarani mkoani Morogoro kimewatahadharisha wananchi wanaotumia usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda na kukaidi kuvaa kofia ngumu kuwa watawajibishwa ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Boniphace Mbao, ametoa tahadhari hiyo, baada ya Oparesheni maalum ya kukagua na kukamata waendesha pikipiki wanaobainika kukiuka baadhi ya sharia, wawapo barabarani hususani kupakia abiria zaidi ya mmoja, pamoja na kutozingatia uvaaji wa kofia ngumu.

Amesema tangu kuanza kwa Oparesheni hiyo mwanzoni mwa mwezi huu jumla ya pikipiki 2,214 zimekamatwa huku waendesha pikipiki 76 wamefikisha mahakamani na wawili kati yao kuhukumiwa kifungo cha miezi mitatu kila mmoja.

Victor Ayo ni mkuu wa kikosi hicho wilaya ya Morogoro anasema elimu imetolewa vya kutosha kilichobaki ni usimamizi wa sheria. Kwa mujibu wa Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani mkoani hapa, Oparesheni hiyo itakua endelevu hadi itakapo bainika kuwa waendesha pikipiki pamoja na abiria wanazingatia sheria zinazo waongoza wawapo barabarani.

Picha na mtandao

Latest News

WATU WATANO WAFARIKI BAADA 'KUSHIKWA MATEKA' KANISANI.
11 Jul 2020 16:57 - Grace Melleor

Watu watano wameuawa baada ya washambuliaji kuvamia kanisa moja Afrika Kusini wakati malumbano yanaendelea juu ya uongoz [ ... ]

RAIS MAGUFULI AMTEUA MAMA SAMIA KUWA MGOMBEA MWENZA.
11 Jul 2020 16:21 - Grace Melleor

Rais Magufuli amemchagua Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea mweza katika Uchaguzi wa Urais wa Tanzania, Oktoba 2020.

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.