Star Tv

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli azindua daraja la Furahisha jijini Mwanza wakati wa ziara yake ya kikazi .

Wakati akiongea na wananchi wa Mwanza rais amesema serikali inafanya jitihada mbalimbali hasa katika kuboresha miundombinu jijini humo ili pawe kitovu cha maendeleo nchini. Utengenezaji wa meli kubwa yenye uwezo wa kubeba watu zaidi ya 1200 pamoja na mizigo,urekebishaji wa meli mbili MV.Victoria na MV.Liyemba,ujenzi wa reli ya standard gage ambayo imekwisha anza Dar es salaam pamoja na upanuzi wa uwanja wa ndege ili uweze kuwa wa kimataifa ni vitu alivyovitaja rais katika mipango ya kuifanya Mwanza kuwa kitovu cha maendeleo.

Ameongeza kua watashirikiana na kampuni kutoka Korea Kusini ambalo limekwiisha wasili nchini wa ajili ya utengenezaji wa meli kubwa.

Lakini pia rais hakuacha kutaja mafanikio yaliyofanywa ambayo ni ujenzi wa daraja la Furahisha pamoja na ujenzi wa barabara ya Usagara na KIsesa ambayo lami imekamilika kwa asilimia 84 na kuwaomba wananchi wa jiji hilo kushirikiana nae ili kufikia lengo ambalo ni kutengeneza Tanzania ya viwanda.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amepewa pongezi kwa jitihada za kimaendeleo anazofanya katika mkoa wake na kutakiwa kukazana hasa kufungua viwanda vilivyokufa mkoani humo.

Picha na mtandao.

Latest News

WATU WATANO WAFARIKI BAADA 'KUSHIKWA MATEKA' KANISANI.
11 Jul 2020 16:57 - Grace Melleor

Watu watano wameuawa baada ya washambuliaji kuvamia kanisa moja Afrika Kusini wakati malumbano yanaendelea juu ya uongoz [ ... ]

RAIS MAGUFULI AMTEUA MAMA SAMIA KUWA MGOMBEA MWENZA.
11 Jul 2020 16:21 - Grace Melleor

Rais Magufuli amemchagua Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea mweza katika Uchaguzi wa Urais wa Tanzania, Oktoba 2020.

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.