Fuvu la kichwa na mabaki ya mwili wa mwanafunzi Alex Pastory wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Nyugwa wilayani Nyang’hwale mkoani Geita kimekutwa kwenye shamba la mwananchi mmoja sababu za kifo chake zikiwa bado hazijafahamika.

 

Hayo yamezungumzwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo wakati akiongea na  Waandishi wa  habari, ambapo amesema marehemu wakati akiwa shuleni akiendelea na masomo kuna wakati aliomba ruhusa ya kwenda Nyumbani kwao ukelewe kwa madai ya kwenda kutibiwa na kutokana na hali yake ya afya kurejea  alirudi shule Februari 28  mwaka huu na kuendelea na masomo.

 

Na kwamba  tangu tarehe 1 mwezi Machi  alitoweka shuleni  na sehemu ambayo alikuwa anaishi kwa kupanga hakuonekana kwani nyumbani kwao ni  Ukerewe  na ilipofika tarehe 8 mwezi huu kuna mwanamke alikuwa akilima shambani ndipo alipoona fuvu la Binadamu huku jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hili ili kujua chanzo cha kifo chake. Hayo yakisemwa na SACP Mponjoli Mwabulambo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita

 

 

Latest News

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:24 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:23 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Chanjo ya Surua Rubella yatolewa Singida.
18 Jun 2019 08:52 - Kisali Shombe

Zaidi ya asilimia 80 ya  watoto  wenye umri wa chini ya miaka mitano, wamepatiwa chanjo ya  Surua Rubella  katika ha [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.