Star Tv

IDARA YA UHAMIAJI Mkoa wa Njombe, kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa imewanasa raia 20 kutoka nchini China ambao ni wafanyakazi wa Kampuni ya ujenzi ya kutoka nchini Korea kwa kuishi na kufanya kazi bila bali vibali.

Kufuatia kwa raia hao kukutwa na kosa la kuishi nchini bila ya kuwa na vibali, kwa mujibu wa Kanuni za idara ya uhamiaji wametozwa faini ya dola za Kimarekani 12,000 yakiwa ni malipo ya Hati Maalum ili waweze kushughulikia vibali vya kuishi na kufanya kazi hapa nchini.

Afisa uhamiaji Mkoa wa Njombe, Kagimbo Hosea amesema oparesheni ya kuwabaini raia hao wa kigeni ilifanyika juzi katika kambi ya ujenzi ya kampuni ya CHEONKWANANG Engineering LTD iliyoko Kata ya Mlangari, inayotengeneza kipande cha barabara ya lami kutoka Lusitu kwenda Mawengi katika barabara kuu ya Njombe-Ludewa na kwamba iwapo raia hao watashindwa kulipa faini hiyo haraka watalazimika kuondoka nchini.

MKUU wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole- Sendeka amesema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa imejiridhisha kuwepo kwa raia hao 20 kutoka China na kuagiza kila mmoja alipe faini ya Dola za Kimarekani 600 ambazo ni kwa mujibu wa Sheria.

Pia ameiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Ludewa pamoja na Kampuni inayojenga barabara hiyo wajiridhishe sifa za vijana wanaopewa silaha za kulinda kufuatia hatua ya mlinzi mmoja kudaiwa kumpiga risasi mfanyakazi dereva wa kampuni hiyo.

Mtuhumiwa anayedaiwa kuhusika kufyatua risasi na kumpiga mfanyakazi mwenzake imelezwa anashikiriwa na Jeshi la Polisi wilayani Ludewa na amefunguliwa kesi ya mauaji baada ya majeruhi huyo kuthibitishwa na mkuu wa wilaya Ludewa amefariki.

Picha na mtandao

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.