Star Tv

Polisi mkoa wa Dodoma linamshikilia John Mwaisango kwa tuhuma za mauaji ya Mhadhiri wa chuo Kikuu cha dodoma Rose Malifred Mndenye ambaye alikuwa ni mke wake katika tukio lililotokea Mei 25 Mwaka huu na kwamba kwa sasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoani hapa Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Gilles Muroto mtuhumiwa huyo amekamatwa akiwa mafichoni katika kijiji cha Chiwachiwa kata ya Mbingu wilaya ya Ifakara mkoani wa Morogoro.

Katika hatua nyingine Jeshi la polisi mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa saba kwa kosa la kujihusisha na usafirishaji wa nyara za serikali kinyume cha sheria ya nchi.

Akitoa taarifa hiyo kamanda wa polisi kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Gilles Muruto amesema watuhumiwa hao wamekutwa na Kobe 536 ambao kati yao kobe 244 ni aina ya Pan Cake na kobe 366 ni aina ya Leopard wenye thamani ya zaidi ya shilingi Mil 84 Za kitanzania.

Amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakikusanya wanyama pori hao kutoka maeneo mbali mbali ya nchi na kuwaleta mkoani Dodoma ambapo huandaliwa na kusafirishwa nje ya nchi .

Aidha kwa mara nyingine, jeshi la polisi linamshikilia msanii wa muziki wa kizazi kipya Rashid Abdalah maarufu kama chidbeenz mwenye miaka 33 mkazi wa Ilala Dar Es Saalam kwa kosa la kukutwa na dawa Za kulevya aina ya bhangi Hii ni mara ya pili kwa msanii huyo kushikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya.

Picha na mtandao

Latest News

Nape Nnauye akutana na Mhe. Rais Magufuli, amuomba radhi.
10 Sep 2019 11:44 - Kisali Shombe

Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi, Mhe. Nape Nnauye amekutana na kumuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza [ ... ]

Mauaji ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini
09 Sep 2019 09:21 - Kisali Shombe

Maafisa wa usalama nchini Afrika Kusini hapo jana walikabiliana na waporaji kwa kutumia magurunedi na risasi za mpira ka [ ... ]

Kura za siri zapigwa kubaini Majambazi na Vibaka, Tabora
09 Sep 2019 09:11 - Kisali Shombe

Wananchi wa wilaya ya Igunga na Nzega mkoani Tabora wameiunga mkono Kampeni ya Fukuafukua Majambazi na Vibaka kwa kupiga [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.