Star Tv

Mradi wa uboreshaji wa taarifa za mabadiliko ya tabia ya nchi na mifumo awali umetumia shilingi bilioni 2.9 kufunga Mitambo ya Hali ya Hewa nchini katika vituo 36.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera Bunge Ajira na watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama amesema katika Bara la Africa ni Nchi mbili pekee zimeweza kufunga mitambo ya kisasa ya kukabiliana na Majanga ya Mabadiliko ya hali ya hewa nazo ni Tanzania na Ethiopia.

Mh. Jenista amesema mitambo hiyo kwa sasa iweze kufanya kazi zaidi kwa kutoa ELimu katika Sekondari kwa kufundisha wanafunzi somo la Jiografia ili kuongeza ufahamu katika kukabiliana na majanga mbalimbali.

Mratibu wa kitaifa wa uboreshaji wa Hali ya Hewa Nchini Tanzania Alfei Daniel amesema mitambo hiyo ya Hali ya Hewa sasa imeunganishwa na simu kwa wakulima ili waweze kufaidika na maumizi ya Kilimo pamoja na kuepukana na Majanga mbalimbali, Naye Brigedia Jeneral Mbazi Msuya amesema Tanzania imesonga mbele katika kukabiliana na Majanga.

Mitambo ya kujua Masuala ya Hali ya Hewa imefungwa katika Vituo 36 kwa Tanzania na mzima na kusababisha kuboresha taifa sahii kutoka asilimia 62% hadi kufikia asilimia67% waziri jenista amesema elimu ya kujua hali ya hewa ina takiwa kila Halimashauri iwe na watu wanao toa tarifa.

Picha na mtandao

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.