Star Tv

Mzunguko wa siku za hedhi kwa wanawake ni jambo ambalo huwa halizungumzwi hadharani katika jamii nyingi barani Afrika kutokana na imani za kidini na kitamaduni.

Vivyo hivyo ushiriki wa wanaume katika suala la hedhi kwa msichana nchini Tanzania lina pande mbili, baadhi wanaunga mkono na wengine wanapingana nayo na kuona kwamba ni suala la siri.

Licha ya kuepo kwa kwa kampeni na harakati nyingi hivi karibuni katika shule na vyombo vya habari bado muamko ni mdogo.

Kampeni hizi zinaibua hisia tofauti miongoni mwa jamii wapo ambao wanachukizwa wakiamini kuwa si jambo sahihi kuzungumzia suala la hedhi hadharani kwasababu tu ya tamaduni kitu ambacho kwa namna moja au nyingine husalia kama kizingiti katika harakati za kuleta uelewa juu ya hedhi hasa kwa vijana.

Wasichana wengi wa sekondari wanakumbana na changamoto kubwa ambayo inaadhiri masomo yao na kufifisha ndoto zao kutokana na kutokuwa katika mazingira mazuri yanayowafanya wawe na hedhi salama.

Maji safi na salama, matundu ya vyoo vya kutosha, walimu walezi wanaojali, bajeti ya kuwezesha shule kununua pedi kwa ajili ya wanafunzi vyote hivyo ni changamoto kwao.

Halima Mohamed kutoka Taasisi ya TAI- Tanzania inayotoa elimu ya hedhi kwa vijana ni muhamasishaji ambaye anahamasisha watu kuchangia pedi huzikusanya na wanazipeleka kwenye shule mbalimbali anasema zoezi hilo linachukua muda mrefu kwa sababu muitikio bado ni mdogo.

Wakati Doreen Temba yeye pia anashiriki katika kutoa pedi bure shuleni,anasema waliamua kufanya shughuli hiyo ili kueza kuwabakiza watoto wa kike shuleni maana huwa wanajisikia aibu kutokana na kukosa kitu cha kujistiri,zamani walikuwa wanatumia khanga,vitenge ambazo zilikuwa hazisaidii.

Hata hivyo sio wanaume wote ambao wamekuwa pembeni katika harakati hizo,Kwa upande wake Kambarage Kasoga anaona kwamba hali hiyo ya hedhi sio jambo la ajabu na jamii anapaswa kutambua kuwa hilo ni jambo la kawaida tu, kwa kuwa kwenye familia au shuleni watoto wa kike wanahitaji msaada kutoka kwa baba na mwalimu pia hata wa kiume.

Huku dunia ikiwa inaadhimisha siku ya hedhi salama,wasichana wanakosa masomo 50 kati ya 194,vipindi 400 kati ya 1552 kwa mwaka kwa mujibu wa takwimu za tafiti zilizofanywa na Mtandao wa jinsia Tanzania(TGNP).

Kwa hisani ya BBC

Latest News

Nape Nnauye akutana na Mhe. Rais Magufuli, amuomba radhi.
10 Sep 2019 11:44 - Kisali Shombe

Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi, Mhe. Nape Nnauye amekutana na kumuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza [ ... ]

Mauaji ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini
09 Sep 2019 09:21 - Kisali Shombe

Maafisa wa usalama nchini Afrika Kusini hapo jana walikabiliana na waporaji kwa kutumia magurunedi na risasi za mpira ka [ ... ]

Kura za siri zapigwa kubaini Majambazi na Vibaka, Tabora
09 Sep 2019 09:11 - Kisali Shombe

Wananchi wa wilaya ya Igunga na Nzega mkoani Tabora wameiunga mkono Kampeni ya Fukuafukua Majambazi na Vibaka kwa kupiga [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.