Star Tv

Kuanzishwa kwa taasisi ya kifedha inayotoa mikopo kwa mwalimu kumetajwa kuboresha maisha ya walimu kutoka hali ngumu waliyokuwa nayo awali na sasa kuishi maisha yenye unafuu.

Inadaiwa kwa sasa kumtofautisha mwalimu na mtumishi mwingine ni kibarua pevu kinachohitaji uchunguzi wa kina, na hiyo ni kutokana na madai ya kuwa maisha ya walimu yapo sawa na watumishi wengine wa serikali, licha ya kuwa bado walimu wanakabiliwa na changamoto mbalimbali, ambapo usaidizi huo wa kimaisha unatajwa ku boreshwa na ujio wa benki ya walimu ambayo inasemekana kuwa chachu ya mabadiliko chanya ya maisha ya walimu.

Stanslaus Muhongole ni mwenyekiti wa chama cha walimu CWT Mkoa wa Iringa kwa upande wake anaona licha ya ujio wa benki ya walimu, lakini bado mwalimu anamahitaji yake muhimu.

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.