Star Tv

Tanzania yatajwa kuwa miongoni mwa nchi zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara zenye viwango vya juu vya Saratani ya Matiti na Shingo ya Kizazi kutokana na kushindwa kujitosheleza katika huduma za uchunguzi wa viashiria vya awali vya wagonjwa wa Saratani ukilinganisha na nchi za Ulaya.

Takwimu za shirika la Kimataifa la Atomiki la Utafiti wa Saratani (IARC) na shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa zaidi ya wagonjwa wapya wa Saratani wanaofikia milioni 14 hugundulika kila mwaka duniani kote na kati yao zaidi ya wagonjwa milioni 8 hufariki dunia. Katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro ambayo kwa miezi kumi sasa imeanzisha kitengo cha Tiba ya Saratani imeeleza kuwepo kwa ongezeko kubwa la wagonjwa wa Saratani.

Katika juma hili la uchunguzi wa awali ili kuzuia ugonjwa wa Saratani ,baadhi ya wataalamu wa idara ya afya kutoka maeneo mabalimbali ya Mkoani Kilimanjaro wamekutana hapa kwa ufadhili wa Benki ya Azania ,lengo ni kupata maarifa zaidi yatakayowaezesha kwenda kutoa huduma stahiki kwa wagonjwa.

Haya yamejiri katika juma la utoaji elimu ya viashiria vya awali vya ugonjwa wa Saratani ,elimu ambayo imeambatana na Mwezi ambao Kimataifa ni Mwezi wa Kumbukumbu ya Ugonjwa wa Saratani ya Matiti dunia kote.

Picha na mtandao

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.