Star Tv

Coca-Cola imetangaza mpango wa kutengeneza kinywaji chenye kilevi kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 125 ya Kampuni hiyo nchini Japan kwa kutumia bidhaa tamu lakini yenye kileo. Bidhaa hiyo ya muundo wa alcopop itakuwa na kiwango cha kileo cha ujazo wa 3% na 8%.

Rais wa Coca Cola nchini Japan Jorge Garduno amesema ''hatujawahi kujaribu bidhaa kama hiyo yenye kileo kidogo, lakini ni mfano wa namna ambavyo tunavyotumia fursa nje ya mipaka yetu''.

Haijafahamika bado kama kinywaji hicho kitauzwa nje ya Japan. Chu-Hi ni kifupi cha Shochu highball ambacho ni mbadala wa bia, maarufu sana kwa wanywaji wanawake.

Kampuni kubwa za vinywaji nchini Japan ikiwemo Kirin, Suntory na Asahi zina aina mbalimbali za vinywaji na wameendelea kufanya majaribio na mamia ya ladha.Lakini mwezi Novemba mwaka jana ilikisiwa kuwa Coca Cola itaanza kutengeneza vileo.

Neno alcopop lina maana ya vinywaji vyenye sukari lakini vyenye kileo, na miaka ya 1990 bidhaa za UK kama vile Hooch, Reef, Smirnoff Ice na Bacardi Breezer zilikuwa maarufu sana. Lakini zilileta mkanganyiko, zikidaiwa zinawafanya vijana kutumia kinywaji chenye kileo kingi kwa kiasi kikubwa kwa kuwa zilikuwa rahisi kutumia.

Latest News

Nape Nnauye akutana na Mhe. Rais Magufuli, amuomba radhi.
10 Sep 2019 11:44 - Kisali Shombe

Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi, Mhe. Nape Nnauye amekutana na kumuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza [ ... ]

Mauaji ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini
09 Sep 2019 09:21 - Kisali Shombe

Maafisa wa usalama nchini Afrika Kusini hapo jana walikabiliana na waporaji kwa kutumia magurunedi na risasi za mpira ka [ ... ]

Kura za siri zapigwa kubaini Majambazi na Vibaka, Tabora
09 Sep 2019 09:11 - Kisali Shombe

Wananchi wa wilaya ya Igunga na Nzega mkoani Tabora wameiunga mkono Kampeni ya Fukuafukua Majambazi na Vibaka kwa kupiga [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.