Star Tv

Halmashauri ya wilaya ya Nyangh’wale mkoani Geita imejikita katika kuboresha zaidi elimu ya Watu Wazima ili kwenda sambamba katika ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia na Tanzania ya viwanda.

Wilaya hiyo kwa sasa ina jumla ya watu wazima 62,054, wanaojua kusoma ni 49,813 na 19,747 hawajui kusoma.

Juma la Elimu ya Watu wazima inaadhimishwa Wilayani humo kauli mbiu ikiwa ni kisomo katika ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia kwa maendeleo ya nchi.

Elimu ya Watu wazima ilianzishwa kwa lengo la kufuta ujinga Halmashauri ina vituo 62 yani kila Shule ya Msingi ni kituo cha Elimu ya watu wazima

Baadhi ya Watu wazima wamejitokeza kujifunza KKK lakini wengi wanaona aibu kwenda kusoma katika vituo.

Kila shule ina Walimu wawili waliopata mafunzo ya KKK ambao wana mbinu za kufundisha watu wazima na wakaelewa vizuri.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Nyanghwale Hamimu Gwiyama amewataka wazazi kuwapa nafasi ya watoto kusoma kwa manufaa ya maisha yao ya sasa na baadaye.

Picha na mtandao

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.