Star Tv

Zaidi ya wakazi laki moja na sabini na moja elfu mia sita hamsini na tatu wilayani serengeti mkoani mara,wanataraji kunufaika na mradi maji safi na afya ya jamii utakaogharimu zaidi ya shilling billion 1.4 kwa kujengewa visima vilefu na vyoo katika vijiji 15 vilivyopo katika kata nne za mosongo,kenyamonta,busawe na machochwe chini ya ufadhili wa kampuni ya cocacola africa foundation.

Wakati sera ya taifa ikitaka kila mwananchi kupata huduma ya maji ndani mita mia nne toka alipo,wakazi wilayani serengeti mkoani mara,bado wanakabiliwa kwa kiasi kikubwa na tatizo la kutokuwa na huduma hiyo muhimu.

Kwa upande wao viongozi katika maeneo hayo,wanasema kuwa tatizo la maji limekuwa likiwakwaza katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Kutokana na hali hiyo,shirika la afya la kimataifa la amref limezindua mradi utakaogharimu zaidi ya sh,billion moja na million mia nne unaotaraji kuvinufaisha vijijini 15 katika kata nne na kuwa fikia wakazi zaidi ya wakazi 171,653.

Akizindua mradi huo mkuu wa wilaya ya serengeti,nourdin babu amewataka wakazi wote watakaokuwepo katika eneo la mradi huo kuhakikisha wanaulinda ili uweze kuwa endelevu. Walengwa wa tasaf wapokea bilioni 20 za tasaf katika kipindi cha miaka miwili mkoani tabora.

Picha na mtandao.

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.