Star Tv
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kuacha kutumia kesi ya kuumwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kama chambo ya kisiasa katika majukwaa. Dr. Mwigulu aliyasema hayo February 13, 2018 mkoani Singida wakati wa kampeni za udiwani katika kata ya Mitunduluni. Amewataka waache kutumia matatizo ya ndugu yao kama mitaji ya kisiasa baadala yake waje na hoja za maana za kusaidia katika maendeleo ya nchi. Aliongeza kusema kuwa mwaka uliopita uhalifu wa ajabu ulitokea ambapo kuna watoto wadogo wa chekechea walitekwa na kuuwawa na wazazi wao ni watu wa kawaida kabisa na kuhoji kama serikali pia imehusika kwenye hilo. “Sisi tunaoshughulika na maswala ya uhalifu tunatafuta wahalifu wanaofanya maswala ya kihalifu, kuna watu wanaona ni agenda ya kisiasa wakati sisi tuombea mtu apone.” Dr. Mwigulu ameongeza kwa kusema kuwa je angeamua kuendelea kusema kuhusu kupigwa risasi kwa mwanajeshi masaki ina uhusiano gani na shida za kata ya mitundulini, hivyo wananchi wa Singida wawaadhibu kwa kuwanyima kura katika uchaguzi wa tarehe 17 mwezi huu.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.