Star Tv

Walengwa wa TASAF wapokea bilioni 20 za TASAF katika kipindi cha miaka miwili mkoani Tabora. 

Zaidi ya wakazi laki 171.653 wilayani serengeti mkoani Mara,wanatarajia kunufaika na mradi maji safi na afya ya jamii utakao gharimu zaidi ya shilling billion 1.4 kwa kujengewa visima virefu na vyoo katika vijiji 15 vilivyopo katika kata nne za Mosongo, Kenyamonta,Busawe na Machochwe chini ya ufadhili wa kampuni ya Cocacola Africa Foundation.

Wakati sera ya taifa ikitaka kila mwananchi kupata huduma ya maji ndani mita mia nne toka alipo,wakazi wilayani Serengeti mkoani Mara bado wanakabiliwa kwa kiasi kikubwa na tatizo la kutokuwa na huduma hiyo muhimu. Kwa upande wao viongozi katika maeneo hayo,wanasema kuwa tatizo la maji limekuwa likiwakwaza katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Kutokana na hali hiyo,shirika la afya la kimataifa la AMREF limezindua mradi utakaogharimu zaidi ya sh,billion moja na million mia nne unaotaraji kuvinufaisha vijiji 15 katika kata nne na kuwafikia zaidi ya wakazi 171,653.

Akizindua mradi huo mkuu wa wilaya ya Serengeti,Nourdin Babu amewataka wakazi wote watakaokuwepo katika eneo la mradi huo kuhakikisha wanaulinda ili uweze kuwa endelevu.

Latest News

Nape Nnauye akutana na Mhe. Rais Magufuli, amuomba radhi.
10 Sep 2019 11:44 - Kisali Shombe

Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi, Mhe. Nape Nnauye amekutana na kumuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza [ ... ]

Mauaji ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini
09 Sep 2019 09:21 - Kisali Shombe

Maafisa wa usalama nchini Afrika Kusini hapo jana walikabiliana na waporaji kwa kutumia magurunedi na risasi za mpira ka [ ... ]

Kura za siri zapigwa kubaini Majambazi na Vibaka, Tabora
09 Sep 2019 09:11 - Kisali Shombe

Wananchi wa wilaya ya Igunga na Nzega mkoani Tabora wameiunga mkono Kampeni ya Fukuafukua Majambazi na Vibaka kwa kupiga [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.