Star Tv
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dr. Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa muda mrefu na zina makosa madogo na kwamba wasikae nazo kwa muda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu. Dr. Mwigulu amesema zile yenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita, dawa ya kulevya wabaki nazo na wafanye utaratibu wa kuwapeleka Mahakamani au kuziteketeza na zenye makosa madogo wazirudishe kwa wamiliki na kuwapa elimu wamekosea wapi. “Wapeni masomo wamekosea wapi, waelekezeni na waliowabishi warekebisheni lakini tusirundike tukatengeza vyuma chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi wake tunao, tutumie huu mkono kwa kutatua yale ambayo yapo ndani ya mamlaka yetu” – Dr Mwigulu Amesema kuwa ipo haja sasa vijana kufundishwa zaidi kuhusu sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za pikipiki na mlundikano wa pikipiki katika vituo vya polisi nchini kwani kila anapopita katika vituo vya polisi hukuta pikipiki nyingi na makosa yao ni madogomadogo.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.