Star Tv

Viongozi na watendaji kwenye Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) wametakiwa kuimarisha vitengo vya ukaguzi wa ndani ili kusaidia usimamizi wa rasilimali fedha kuhakikisha kuwa fedha zinazoingia na kutumika zinatumika ipaswavyo kulingana na bajeti.

Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma na mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa kufunga semina ya siku mbili baina ya wataalamu viongozi na watendaji kutoka mamlaka hizo waliokuwa wakishiriki kupokea na kuchangia taarifa ya tathmini ya utekelzaji wa ugatuzi wa madaraka na sekta ya umma nchini.

Mwanri amesema, kutokana na wingi wa fedha unaotumwa kwenye halmashauri ni vigumu kwa viongozi kufahamu fedha zilizoingia na namna zinavyotumika bila kuwatumia wakaguzi wa ndani mara kwa mara. Naibu katibu mkuu ofisi ya rais utumishi wa umma bi. Susan Mlawi amesema kuwa lengo la mjadala huo ni kushirikisha wadau wote kutoa maoni yatakayotumika kuboresha sera na mifumo ya uendeshaji wa ugatuzi wa madaraka na usimamizi wa sekta ya umma katika utendaji na utoaji wa huduma kwa jamii.

Kutokana na ugatuzi wa madaraka kwa dhana kuwa na lengo la kusogeza madaraka kwa wananchi toka ngazi ya kijiji Paschal Nkwabi amezungumza na muwezeshaji wa semina hiyo profesa Prosper Ngowi kujua endapo mfumo huo unatija katika maendeleo kwa ujumla ikiwemo kupunguza umaskini miongoni mwa watanzania.

Wakati wa ufunguzi wa semina hiyo waziri ofisi ya rais tamisemi Selemani Jafo aliwataka washiriki hao kuwa na mpango wenye tija ili kuhakikisha kuwa maoni yao yatasaidai kuifanya sera ya ugatuzi wa madaraka na uimarishaji wa utendaji sekta ya umma kwe nye utoaji wa huduma za jamii inchini. 

Picha na mtandao

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.