Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema serikali itawachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha kazi watumishi wa idara ya uvuvi na maafisa uvuvi kwenye halmashauri zote nchini watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu katika kutokomeza uvuvi haramu.

Zaidi ya watu milioni tatu wameendelea kunufaika na sekta ya uvuvi katika ziwa victoria ikiwemo uchakataji wa samaki, utengenezaji wa zana na vyombo vya uvuvi, pamoja na biashara ndogondogo.

Licha ya serikali kuendelea kupambana na changamoto ya uvuvi haramu ili kuhakikisha rasilimali za uvuvi zinaboreka bado baadhi ya watendaji wa serikali ni kikwazo.

Waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina anabainisha hilo katika zoezi la kuteketeza zana haramu za uvuvi zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 450 kwenye kijiji cha Kageye wilayani Magu mkoani Mwanza zilizokamatwa katika operesheni ya siku tano kwenye Wilaya hiyo na Wilaya Busega mkoani Simiyu Aidha ameitaka jamii kujiepusha na uvuvi haramu kwani serikali haiko tayari kumvumilia mtu yeyote ataye jishughulisha na shughuli hiyo.

Hata hivyo wakuu wa Wila za Magu na Busega pamoja na wadau wa uvuvi wamesema zoezi hilo ni endelevu. Katika oparesheni ya kudhibiti uvuvi haramu iliyofanyika katika wilaya hizo mbili jumla ya shilingi milioni 125 zimepatikana baada ya wavuvi kutozwa faini kutokana na makosa mbalimbali ya Uvuvi.

Picha na mtandao.

Latest News

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:24 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:23 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Chanjo ya Surua Rubella yatolewa Singida.
18 Jun 2019 08:52 - Kisali Shombe

Zaidi ya asilimia 80 ya  watoto  wenye umri wa chini ya miaka mitano, wamepatiwa chanjo ya  Surua Rubella  katika ha [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.