January 15, 2018 Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ametoa taarifa inayoelezea mambo aliyoyajadili wakati alipokwenda IKULU kukutana na Rais Magufuli January 9 2018.

Baada ya kutoka IKULU hiyo January 9 Lowassa alisifia utendaji kazi wa Rais Magufuli kwa aliyoyafanya toka ameingia madarakani ambapo alitaka pia Watanzania waendelee kumuunga mkono.

Taarifa ya Lowassa ya leo inanukuliwa ikiwa imeandikwa yafuatayo

 “Mnamo January 9 2018 nilipokea mwaliko kutoka kwa Rais Dr. John Pombe Magufuli akiniomba kwenda kukutana nae IKULU siku hiyohiyo kwa ajili ya mazungumzo“

Aidha, Jumapili January 14 2018 nilipata fursa ya kukielezea kwa kina Chama changu kupitia kikao cha kamati kuu ya mazungumzo yangu na Rais Dr. Magufuli IKULU, ujumbe wa Rais Magufuli kwangu ulikua ni kunishawishi nirejee CCM suala ambalo sikukubaliana nalo

Na nilimueleza Rais ya kwamba uamuzi wangu wa kukihama chama hicho na kujiunga CHADEMA haukuwa wa kubahatisha” – Edward Lowassa.

Latest News

Mauaji ya kukata makoromeo, washtakiwa wahukumiwa. Bukoba
20 Jun 2019 08:21 - Kisali Shombe

MAUAJI YA KUKATA MAKOROMEO:Washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Mahakama kuu kanda ya Bukoba  imewahukumu  kunyo [ ... ]

Kudorola kwa soko la Pamba.
19 Jun 2019 12:20 - Kisali Shombe

Madiwani halmashauri ya wilaya ya bariadi mkoani Simiyu wameilalamikia serikali kuhusu zao la pamba kukosa soko la uhaki [ ... ]

Adha ya maji, Kalambo
19 Jun 2019 11:23 - Kisali Shombe

Wananchi  katika   kjiji cha  Kisungamile  kata  ya  matai   wilayani  Kalambo  mkoani  Rukwa  wameiomba   [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.