Star Tv

Uzinduzi wa upigaji chapa mifugo umefanyika mkoani Songwe wafugaji wakishauriwa kufuga idadi ndogo ya mifugo ili kuondoa kero wanayokutana nayo katika kutafuta malisho na kusababisha migogoro baina ya wakulima na wafugaji.

Uzinduzi wa kupiga chapa Mifugo umefanyika katika Kata ya Mbuyuni kijiji cha Ndanga ambapo Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa amezindua shughuli hiyo na kuwataka wafugaji kufuga mifugo yao kisasa na kwa tija badala ya ilivyo hivi sasa.

Katika taarifa ya umoja wa wafugaji iliyosomwa na Josephath Jackson imeeleza kuwa wafugaji hao wanakabiliwa na changamoto ya malisho, soko la maziwa na kwamba serikali iwasidie kupata masoko ya maziwa wanayozalisha.

Shughuli ya upigaji Chapa Mifugo inapokelewa vyema na wafugaji mbalimbali na kuishukuru serikali kwa kuanzisha mfumo huo.

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.