Star Tv

Butiama inayotajwa kuwa moja ya vivutio vikubwa vya utalii nchini imeonekana kutelekezwa ambapo miundombinu isiyokidhi na uhaba wa maji vinatajwa kulikabili eneo hilo.

Utalii umekuwa ukichangia asilimia 17 ya pato la Taifa na asilimia 25 ya fedha za kigeni. Inawezekana historia kufutika, au uzito wa historia hiyo kupungua kutokana na changamoto zinazolikabili eneo la Butiama na kijiji cha mwitongo mkoani Mara kinachoonekana kama eneo lililotelekezwa.

Uhaba wa maji, miundombinu isiyokidhi katika eneo hilo la kihistoria nchini, na maisha ya mwalimu nje ya siasa ni masuala yanayowakutanisha wanahabari kutoka klabu ya waandishi wa habari Mwanza na Mtoto wa 6 wa muasisi wa Taifa hili Madaraka Nyerere katika kipindi cha tujadiliane Tukiihuisha historia ya nchi hii kwa kumtaja mwl Nyerere, na pengine ni vigumu kumtaja mwalimu vizuri bila kusikia historia kutoka kwa mtu wa karibu na hasa watoto wake.

Madaraka amesema katika kipindi cha urais hawakuishi muda mrefu katika ikulu bali maisha yao waliyaendesha wakiwa uraiani kama watoto wengine na baba yao. Madaraka amewaasa vijana kuwa na uvumilivu wa kisiasa kama aliokuwa nao mwalimu, wakati huohuo Mkurugenzi wa umoja wa klab za wanahabari Tanzania UTPC anaona umuhimu wa serikali kuangalia upya na kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto zinazolikabikli eneo la butiama na kuwahimiza wanahabari kuhakikisha changamoto hizo zimefanyiwa kazi.

Aliakisi ualimu na ubaba wa Taifa, huyu mpigania uhuru wa Tanganyika na raisi wa kwanza wa Tanzania JULIUS KAMBARAGE NYERERE .

Picha na mtandao.

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.