Utelekezaji wa watoto kwa mabinti na wanawake na kuwaacha kuishi katika mazingira hatarishi imekuwa changamoto inayosababisha ongezeko la watoto wanaolelewa katika vituo vya kulelea watoto yatima.
Baadhi ya vituo vinadaiwa kukosa uwezo wa kuwalea kutokana na kuelemewa na idadi kubwa ya watoto.
Kituo cha Faraja Ophanage childrens home kinatunza watoto zaidi ya 200 waishio katika mazingira hatarishi ambapo 30 kati yao wanaishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi huku changamoto kubwa ikiwa ni ukosefu wa lishe kwa watoto hawa.
Kupitia changamoto zinazowakabili watoto hawa wadau mbalimbali wanaona kuna umuhimu wa kuungana nao hasa katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwapatia mahitaji ya vyakula
Miongoni mwa vitu vilivyotolewa na wadau hawa kwa ajili ya watoto wa kituo cha Faraja ni pamoja na mahindi,mafuta,mchele nguo sabuni huku wadau mbalimbali wakihimizwa kujitokeza kuungana na watoto hawa hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu.
Picha na mtandao.