Star Tv

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo Oktoba 19,2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Uchumi na Biashara za kimataifa wa Ufaransa Franck Riester, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Katika Mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine Waziri Riester ameleta salamu maalum pamoja na mwaliko Rasmi wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Waziri Riester amesema Ufaransa inatambua jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania ikiwemo kuboresha mazingira ya biashara pamoja na kuleta usawa wa kijinsia
mambo ambayo pia yanatiliwa mkazo na serikali ya Ufaransa.

Amesema Ufaransa imedhamiria kuongeza ushirikiano na Tanzania kwa manufaa ya nchi zote mbili huku akitoa mfano wa kuanzishwa kwa usafiri wa ndege wa moja kwa moja kutoka Paris Nchini Ufaransa hadi Zanzibar ulioanza hivi karibuni ambao ulisimama kwa miaka 47.

Waziri huyo wa Uchumi wa Ufaransa ameambatana na Wafanyabiashara mbalimbali kutoka Ufaransa wenye nia ya kuwekeza nchini.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Ufaransa na kuwahakikishia Tanzania ni Nchi salama kuwekeza iliiyojaliwa rasilimali nyingi na fursa lukuki.

Amesema pamoja na changamoto za kiuchumi zilizosababishwa na Uviko 19, serikali imeendelea kuchukua jitihada mbalimbali kupambana na hali hiyo ikiwemo kutoa chanjo ili kukabiliana na ugonjwa huo.

Aidha amesema Ufaransa imekuwa kati ya wadau wakubwa wa maendeleo nchini Tanzania na uwekezaji katika sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo ujenzi wa Miundombinu, Elimu pamoja na Maji huku akiwakaribisha kuwekeza katika sekta ya Afya hususani ujenzi wa viwanda vya dawa, sekta ya Utalii na Nishati.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mawaziri kutoka serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania.

Latest News

SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA LAUA WATU NANE SOMALIA.
25 Nov 2021 10:26 - Grace Melleor

Polisi nchini Somalia wamethibitisha vifo vya raia katika bomu lililotegwa ndani ya gari katika mji mkuu Mogadishu, tele [ ... ]

WAZIRI MKUU SWEDEN AJIUZULU SAA CHACHE BAADA YA KUTEULIWA.
25 Nov 2021 09:01 - Grace Melleor

Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke kuwahi kushikilia wadhifa huo nchini Sweden amejiuzulu saa chache mara baada ya kuteuliwa [ ... ]

MTOTO WA GADDAFI AZUIWA KUGOMBEA URAIS LIBYA.
25 Nov 2021 07:13 - Grace Melleor

Mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania uchaguzi wa  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.