Star Tv

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri.

Mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri ni pamoja uteuzi mpya wa mawaziri watatu kwa kutengua waliokuwepo pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi.

Miongoni mwa sura mpya katika baraza hilo la mawaziri, ni mbunge aliyemteua siku chache zilizopita Dokta Stergomena Tax ambaye amemteua kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa nchini Tanzania.

Wizara zilizokutana na mabadiliko hayo, ni Wizara ya Habari kuondolewa, kutoka katika Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo na sasa itakuwa katika Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Rais Samia pia amemteua Dokta Eliezer Feleshi kuwa mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuchukua nafasi ya Profesa Adelardus Kilangi aliyeteuliwa kuwa balozi.

Latest News

UFARANSA YAZINDUA MAGARI YA UMEME HAPA NCHINI.
20 Oct 2021 15:31 - Grace Melleor

Waziri wa Biashara na uchumi nchini Ufaransa Franck Riester amezindua magari ya umeme yaliyoundwa na kampuni ya E-Motion [ ... ]

UHITAJI WA NYAMA WAONGEZEKA NCHINI.
20 Oct 2021 15:23 - Grace Melleor

Serikali imesema malalamiko yaliyojitokeza hivi karibuni ya kupanda kwa bei ya nyama nchini yanaashiria ukuaji wa sekta  [ ... ]

UGANDA YAZINDUA GARI LA KIVITA LILILOUNDWA NCHINI HUMO.
19 Oct 2021 18:03 - Grace Melleor

Jeshi la Uganda limezindua gari la kivita lililoundwa nchini humo.

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.