Star Tv

Jaji Elinaza Luvanda wa Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa na aliyekuwa anaisikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi namba 16/2021 inayomkabili Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe na wenzake watatu amejitoa kusikikiza kesi hiyo.

Mapema leo jijini Dar es Salaam, Mbowe akiwawakilisha wenzake watatu alimuomba Jaji Luvanda aliyekuwa akiendesha kesi hiyo ya ugaidi kujitoa kwa madai kuwa hawana imani naye na kwamba hatotenda haki.

Hata hivyo Jaji Luvanda alitangaza kujitoa kuisikiliza na kesi hiyo kuahirishwa ikisubiri jaji mwingine apangiwe.

Mbowe na wenzake walipofikishwa mahakamani leo, hatma ya mapingamizi yao dhidi ya hati ya mashtaka iliyotumika kuwafungulia kesi ya kula njama za kufanya ugaidi ilipata majibu huku ombi la moja likikataliwa.

Aidha, Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alisema, “Mahakama imekataa pingamizi moja, na lingine wamelikubali kwa kiasi fulani na kusema kuwa upande wa mashataka wanapaswa kurekebishe kasoro.

Hata hivyo hatujafurahi kwa sababu tulitaka mashtaka hayo yafutwe.” Mbowe na wenzake watatu wanashikiliwa tangu Julai 21, wakikabiliwa na kesi ya ugaidi.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.