Star Tv

Mgombea urais wa chama cha ACT Wazalendo kwa upande wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesimamishwa kufanya kampeni na Kamati ya maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar- ZEC kwa muda 5.

Adhabu hiyo imetolewa hii leo Octoba 16, baada ya kamati hiyo kukaa na kusikiliza malalamiko yaliyo wasilishwa na Chama cha Demokrasia Makini ambapo imemtuhumu mwanasiasa huyo mkongwe kwa kuhamasisha watu kujitokeza na kupiga kura tarehe 27 ambayo kwa mujibu wa sheria imetengwa kwa watu maalumu.

ACT Wazalendo kimeituhumu Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kwa kuwa na upendeleo, Akizungumza na BBC Afisa wa habari na uenezi Salim Bimani amesema;

"Tume ya uchaguzi wa Zanzibar ZEC inatumika na inatumika vibaya dhidi ya chama cha ACT Wazalendo, tuna ushahidi kwasababu masuala mengi ambayo tumekuwa tukiyadai, tukiyaeleza na kuyalalamikia tume hata siku moja haijapata kujibu, hauijapata kutekeleza, taijapata kuwa wazi, kile kinachotakikana kwenye CCM ndicho wanachokifanya"- Bimani.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi Zanzibar Thabit Faina ameiambia BBC kwamba mgombea huyo wa ACT Wazalendo anaweza kukata rufaa.

Aidha, kwa upande wa chama cha ACT Wazalendo wamesema watakaa kesho na kulijadili kabla hawajalitolea maamuzi.

Chanzo: bbc Swahili.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.