Star Tv

Panya mkubwa kutoka Afrika amepewa nishani ya dhahabu kutokana na uwezo wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini.

Panya huyo anayejulikana kwa jina la Magawa ameweza kunusa mabomu 39 na silaha 28 ambazo hazijalipuka katika maisha yake.

Shirika la matibabu ya wanyama la Uingereza lisilokuwa la kiserikali PDSA limemtuza medali ya dhahabu "kwa kujitolea kwake kuokoa maisha kupitia kazi yake ya kubaini mabomu hatari yaliyotegwa ardhini Cambodia".

Inadhaniwa huenda kuna hadi mabomu milioni sita ya kutegwa ardhini katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa bara Asia.

Nishani ya dhahabu ya PDSA, imeandikwa maneno haya "Kwa juhudi za wanyama au kujitolea kazini ", Na kwa wanyama 30 waliopewa tuzo hiyo, panya huyu ni wa kwanza.

Panya huyo aliye na miaka saba alipewa mafunzo na shirika lisilo la kiserikali- Apopo kutoka Ubelgiji lenye makao yake nchini Tanzania. Shirika hilo limekuwa likiwalea wanyama wanaofahamika kama - PanyaShujaa- kugundua uwepo wa mabomu ya kutegwa ardhini tangu miaka ya 1990.

"Ni heshima kubwa kwetu kupokea tuzo hii, Lakini pia ni ushindi mkubwa kwa watu wa Cambodia, na watu wengine duniani ambao wamekuwa wakiteseka kutokana na mabomu ya kutegwa ardhini."-Afisa Mkuu Mtendaji wa Apopo, Christophe Cox aliambia shirika la habari la Press Association.

Kulingana na Apopo, Magawa - alizaliwa na kulelewa Tanzania - akiwa na uzani wa kilo 1.2 (2.6lb) na urefu wa senti mita 70 (28in), Japo ni mkubwa kuliko spishi zingine za panya, Magawa ni mdogo ni mwepesi kiasi kwamba hawezi kulipua mabomu akitembea juu.

Magawa ana uwezo wa kusaka mabomu katika eneo lenye ukubwa wa uwanja wa mpira wa tennis kwa muda wa dakika 20 - jambo ambalo Apopo linasema itamchukua mtu aliye na kifaa cha kubaini vifaa vya chuma kati ya siku moja hadi nne.

Panya huyo anafanya kazi kwa saa moja na nusu kwa siku nyakati za asubuhi na anakaribia kustaafu, lakini Mkurugenzi Mkuu wa PDSA Jan McLoughlin amesema kazi yake katika shirika la Apopo ilikuwa "ya kipekee na ya kuridhisha".

Panya kama Magawa wanafundishwa kubaini kemikali iliyotumiwa katika vilipuzi, kumaanisha wanaweza kupuuza vyuma vikuukuu na kutafuta mabomu kwa haraka zaidi na wanapopata kilipuzi wanakuna juu yake na kuwaonesha binadamu wafanyakazi wenzao.

Kazi ya Magawa inaokoa na kubadilisha maisha ya binadamu ambao wanaathiriwa na mabomu hayo ya kutegwa ardhini," aliambia shirika la hapari la Press Association. "Kila uvumbuzi anaopata unapunguza hatari ya kujeruhiwa au kufariki kwa watu."

Chanzo: BBC Swahili.

 

Latest News

ETHIOPIA YASEMA HAITISHWI NA TAMKO LA RAIS DONALD TRUMP.
24 Oct 2020 16:54 - Grace Melleor

Waziri mkuu wa Ethiopia amesema nchi yake "haitakubali vitisho vya aina yoyote" baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa M [ ... ]

RAIS TSHISEKEDI ATANGAZA MASHAURIANO YA UMOJA KWA MUUNGANO TAWALA.
24 Oct 2020 06:41 - Grace Melleor

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, katika hotuba yake kwa taifa aliyoitoa siku ya Ijumaa wiki hi [ ... ]

SEKTA YA AFYA NCHINI YAPATA NEEMA KUTOKA USWISI.
23 Oct 2020 15:23 - Grace Melleor

Serikali imepokea msaada wa Faranga za Uswisi Milioni 15.75 sawa na shilingi Bilioni 39.59 kwa ajili ya kugharamia mradi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.