Star Tv

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameitisha kikao na baraza la ulinzi nchini mwake kufuatia Shambulio la Koure nchini Niger.

Hii ni baada ya shambulio ambalo liligharimu maisha ya wafanyakazi sita wa shirika la misaada ya kibinadamu kutoka Ufaransa na wenzi wao wawili kutoka Niger, rais wa Ufaransa ameitisha kikao cha baraza la ulinzi kutathmini hali mbambo kuhusu shambulio hilo.

Rais Emmanuel Macron ataongoza kikao hicho cha Baraza la Ulinzi kwa njia ya video. Atawakusanya pamoja Waziri Mkuu Jean Castex, Mawaziri wa Mambo ya nje, Ulinzi na Mambo ya ndani, na pia wakurugenzi na waratibu wanaohusika, hasa idara ya ujasusi.

 Wakati huo huo jeshi la Niger, likisaidiwa na lile la Ufaransa wameanzisha msako wa kuwatafuta watu waliotekeleza mauaji ya watu wanane wakiwemo watalii sita kutoka nchini Ufaransa.

 Nao wachunguzi nchini Ufaransa wameanzisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo yaliyotokea Jumapili iliyopita katika mji wa Koure, huku serikali ya Niger na Ufaransa wakiapa kuwapata waliohusika na mauaji hayo.

 Mapema Jumatatu hii Paris ilithibitisha kwamba Wafaransa hao waliuawa katika shambulio hilo lililotokea Jumapili. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia alizungumza kwa simu na mwenzake wa Niger, Mahamadou Issoufou, Ikulu ya Elysee alisema.

 Rais wa Ufaransa na mwenzake wa Niger waliapa kuendelea na vita dhidi ya makundi ya kigaidi huko Sahel.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.