Star Tv

Leo Japan inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 75 ya shambulizi la bomu la atomiki katika historia yake.

Shambulizi hilo la bomu la atomiki lililotekelezwa kwa mara ya kwanza duniani lilisababisha maafa makubwa na kuharibu miji iliyopakana na Hiroshima na kupelekea vifo vya watu 70,000, Bomu la pili la aina hiyo liliangushwa Nagasaki siku tatu baadaye.

Imepita miaka 71 tangu Japan kukumbwa na maafa ya Hiroshima yaliyosababishwa na bomu la atomiki lililorushwa na Marekani tarehe 6 Agosti mwaka 1945 wakati wa vita vya pili vya dunia.

Wajapan wameendelea kuwa na hofu kubwa kutokana na janga la Corona na kusababisha kusahau yaliyotokea katika miji wa Hiroshima na Nagasaki. Sherehe za kuwakumbuka wahanga wa tukio hilo huko Hiroshima zimefutwa. Virusi hivyo huzuia watoto wa shule za Japan kutoka kwa makundi kutembelea Bustani ya Amani, jumba lake la ukumbusho lililojengwa kwenye kitovu cha mlipuko wa bomu hilo la atomiki, 'jumba la kumbukumbu'.

Majira ya saa mbili na robo asubuhi ya tarehe 6 Agosti 1945, ndege ya kijeshi ya Marekani chapa B-29 Enola Gay iliangusha bomu lililopewa jina la "Mvulana Mdogo" na kuwauwa hapo hapo watu 140,000 kati ya wakaazi 350,000 wa mji huo.

Maelfu ya watu wengine walikufa siku za baadaye kutokana na majeraha na mionzi ya atomiki. Alkhamis ya leo, katika muda huo huo bomu hilo liliporipuka, watu walisimama na kunyamaza kimya kwa muda kuwakumbuka wahanga hao.

Waziri Mkuu Shinzo Abe alihudhuria kumbukumbu hiyo kama kawaida, lakini wageni kutoka jumuiya ya kimataifa walikuwa wachache.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.