Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kwamba "janga la Corona linaongezeka kwa kasi" na kukiri kwamba "ushahidi unaonyesha" kuwa kuna uwezekano virusi vya Corona kusambazwa kwa njia ya hewa.
Kauli hiyo inakuja baada ya kundi la wanasayansi 239 wa kimataifa kutoa tahadhari kuhusu njia hii ya maambukizi.
Zaidi ya wanasayansi 200 wa kimataifa wameitaka WHO na jamii ya kimataifa ya matibabu "kutambua uwezekano wa maambukizi ya virusi vya Corona kwa njia ya hewa," katika barua ya wazi iliyochapishwa Jumatatu katikaGazeti la Magonjwa ya Kuambukiza, Clinical Infectious Diseases, ya huko Oxford.
Hoja ambayo Shirika la Afya Duniani linapaswa kuchunguza, kwa mujibu wa Isabella Annesi-Maesano, moja wa wanasayansi hao waliotia sani kwenye barua hiyo. Ni mkurugenzi wa utafiti katika Inserm, mtaalam wa magonjwa ya kuambukia na magonjwa ya kupumua.
Shirika la Afya Duniani linasema hakuna ushahidi, lakini nataka kusema kwamba kukosekana kwa ushahidi sio dhibitisho la kutokuwepo. Nina maanisha kwamba kuna data nyingi na hata ikiwa hakuna data kama hiyo WHO wanapaswa kuwa waangalifu, Profesa Isabella Annesi-Maesano, amesema katika mahojiano na Valérie Cohen.
"Tunatambua kuwepo na ushahidi na tunapaswa tuwe wazi kwa uwezekano huu na kuelewa athari zake," amesema Benedetta Allegranzi, afisa wa WHO, katika mkutano na waandishi wa habari.