Star Tv

Kampuni ya mtandao wa kijamii ya Facebook imeondoa mtandaoni matangazo ya kampeni ya rais Donald Trump kwa kile kinachoelezwa kuwa ametumia alama zilizokuwa za utawala wa kinazi wa Ujerumani.

Facebook imesema tangazo lililolengwa lilikuwa na alama ya pembe tatu nyekundu kama iliyotumika na utawala wa kinazi kuwatambua wapinzani wao kama wakomunisti.

Timu ya kampeni ya Trump imesema kuwa tangazo hilo lilikuwa linakilenga kikundi cha wanaharakati wa mrengo wa kushoto antifa, ambacho wanadai kinatumia nembo hiyo. Huku upande wa Facebook inadai matangazo hayo yanaenda kinyume na sera yake ya chuki ya kupangwa.

"Haturuhusu alama ambazo zina simama kwa mirengo ama makundi ya chuki, labda iwe ni kukemea jambo hilo, Hiko ndicho tulichokiona kwenye tangazo hili, na popote pale alama hiyo itakapotumika tutachukua hatua kama hii," ameeleza mkuu wa sera za ulinzi wa Facebook Nathaniel Gleicher.

Matangazo hayo, ambayo yaliwekwa kwenye kurasa za mtandao wa Facebook za Trump na Makamu wake Mike Pence yalifutwa baada ya kuwa mtandaoni kwa saa 24. "Pembe tatu nyekundu ni alama inayotumiwa na antifa, hivyo ilitumika katika tangazo kuhusu antifa," ameeleza Tim Murtaugh, msemaji wa timu ya kampeni ya Trump.

Rais Trump katika siku za hivi karibuni amelishutumu kundi la antifa kwa kuanzisha maandamano ya vurugu kote nchini Marekani kufuatia kifo cha mtu mweusi George Floyd mikononi mwa polisi.

Rais Trump alitishia mwezi uliopita kuwa atalitangaza kundi hilo linalopingana na itikadi za kifashisti kuwa "kundi la kigaidi la ndani ya nchi", ijapokuwa wataalamu wa sheria hawana hakika kama ana uhalali wa kufanya hivyo. Antifa ni kundi la maandamano la mrengo mkali wa kushoto ambalo linapingana na unazi, ufashisti, ukimya wa weupe na ubaguzi wa rangi.

Linatajwa kuwa ni kundi lisilo na uongozi maalumu, na waandamanaji wake wanapinga sera za Trump dhidi ya uhamiaji, utaifa na Waislamu.

Aidha, Matangazo hayo ni sehemu ya kampeni ya Trump kwa uchaguzi wa Novemba mwaka huu.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.